
Klabu ya Al Ahly SC 🇾🇪 ya Misri imethibitisha kumteua mkufunzi Hussein Ammouta kuwa kocha mkuu mpya kwa mkataba wa miaka miwili akichukua mikoba ya Jess Thorup aliyeachishwa kazi kwa makubaliano ya pande zote mbili mapema mwezi huu.
Ammouta 56, raia wa Morocco🇲🇦 anatua klabuni hapo akiwa na uzoefu mkubwa kwenye soka la Afrika kwani mwaka 2017 aliiongoza Wydad Casablanca kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly🔴⚪🇾🇪✅🔐
