
🚨🎙️Kinda anayekimbiza kwa sasa, Ayyoub Bouaddi, ameweka wazi mapenzi yake ya tangu utotoni kwa klabu ya Manchester United na kukiri kuwa ni ndoto ya kila mchezaji kuvaa uzi wa mashetani hao wekundu.
Katika mahojiano yake, Bouaddi alisema:
🗣️ “Nilikuwa nikiitazama Manchester United kwa karibu sana nilipokuwa mtoto, mimi ni shabiki mkubwa wa klabu hiyo.”
🗣️ “Ndio kwanza ninaanza misingi yangu na siko kwenye haraka, lakini kwa namna yoyote ile, ile ni Manchester United! Ni ndoto ya kila mchezaji kucheza pale.”
