

Mshambuliaji wa Real Madrid, Kylian Mbappe ameshinda tuzo ya mfungaji bora wa msimu wa Ligi Kuu Uhispania, Laliga ‘pichichi’ kwa msimu wa pili mfululizo baada ya kufunga magoli 25 baada kwenye michezo 29 ya Laliga msimu huu.
Mbappe amekuwa mchezaji wa kwanza wa Real Madrid kutwaa tuzo ya pichichi mara mbili mfululizo tangu Cristiano Ronaldo afanye hivyo msimu ya 2014/15 na anakuwa mchezaji wa kwanza kufanya kwenye Laliga tangu Messi achukue tuzo hiyo kwa mara ya pili mfululizo msimu wa 2020/21.
Kwingineko Mabingwa wapya wa Laliga, Barcelona wamemaliza msimu kwa kichapo cha 3-1 dhidi ya Valencia kwenye mchezo wa mwisho wa Ligi hiyo huku Real Madrid ikifunga msimu kwa ushindi mnono wa 4-2 dhidi ya Athletic Bilbao.
FC Barcelona, Real Madrid, Villarreal, Atletico Madrid na Real Betis zimemaliza katika nafasi tano za juu kwenye msimamo wa Laliga na kujihakikishia kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.


