

Baada ya miaka miwili nje ya benchi la ufundi, Jürgen Klopp amerejea rasmi kwenye ukocha baada ya kusaini mkataba wa kuinoa timu ya taifa ya Ujerumani hadi Julai 2030.
Shirikisho la Soka la Ujerumani limethibitisha kufanyika kwa makubaliano hayo, huku tangazo rasmi likitarajiwa kutolewa leo.
Klopp, ambaye alijijengea sifa kubwa akiwa kocha wa Liverpool, sasa anakabidhiwa jukumu la kuiongoza Ujerumani katika enzi mpya, akilenga kurejesha makali ya timu hiyo kwenye mashindano makubwa ya kimataifa.
Baada ya kusubiri kwa miaka miwili, “Kloppo” amerudi rasmi, na mashabiki wa soka duniani wanasubiri kuona atakavyoandika historia mpya akiwa na Die Mannschaft. 🇩🇪🧢

