Patrick Simon, mdau wa soka nchini Tanzania, ametoa maoni yake kuhusu hali ya timu ya Taifa Stars, akisema:
“Kama viongozi wanaosimamia timu hii ya Taifa Stars, kwa kweli timu hii ni mbovu sana. Asilimia 80 ni mbovu na inatupa aibu sisi Watanzania. Haya ni mawazo yangu, lakini kama yatawapendeza, mnaonaje twende tuchukue timu ya U-17 iliyocheza fainali ya AFCON U-17, kama bado wapo, waingizwe kwenye mashindano ya Championship, Azam Federation Cup, Mapinduzi Cup na mashindano yote yanayozikutanisha timu za Ligi Kuu.
AFCON ikifika, tuwaongezee wachezaji wakongwe watano wenye exposure na uzoefu wa kimataifa ili wakatuwakilishe AFCON.”


