

FC Barcelona imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu Uhispania (Laliga) kwa mara ya pili mfululizo kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya mahasimu wao wakubwa, Real Madrid kwenye mchezo wa El Clasico katika dimba la Nou Camp.
Barca imetwaa ubingwa huo kwa mara ya 29 kihistoria kwa namna ya kipekee kwani imetwaa ubingwa huo baada ya kuwafunga mahasimu wao hao na ni kwa mara ya kwanza bingwa wa Laliga amepatikana kwenye mchezo wa El Clasico.
FT: Barcelona 2-0 Real Madrid
⚽ 09′ Rashford
⚽ 18′ Torres



