
Kiiungo fundi Kelvin Nashon Naftal anatajwa kukamilisha dili la kujiunga na Simba SC kutoka Pamba Jiji kwa ajili ya msimu ujao. Taarifa mbalimbali zinaeleza kuwa mazungumzo yamefikia hatua nzuri sana huku kiungo huyo akitarajiwa kuvaa jezi nyekundu na nyeupe ya Wekundu wa Msimbazi.
Kelvin Nashon ni aina ya viungo ambao wana nguvu ya kukaba, uwezo mzuri wa kupandisha mashambulizi na nidhamu kubwa ndani ya uwanja. Kwa misimu ya hivi karibuni ameonyesha kiwango kizuri sana kwenye ligi, jambo ambalo limefanya timu kubwa kuanza kumfuatilia kwa karibu.
Faida kubwa kwa Simba ni kupata kiungo mzawa mwenye uzoefu wa ligi ya Tanzania, kitu kitakachosaidia kuongeza ushindani mkubwa eneo la kiungo hasa kwenye mechi za presha kubwa za ligi na michuano ya CAF.
Kama ataendelea na kiwango chake na kupata mazingira mazuri ndani ya Simba, basi ana uwezo mkubwa wa kuwa mmoja wa viungo bora wazawa nchini msimu ujao.


