Kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Allan Okello amefunguka kuhusu mjadala unaoendelea kati yake na kiungo wa Simba SC, Clatous Chama huku akisisitiza hana ushindani binafsi na staa huyo wa Zambia.
Okello amesema anamfahamu Chama tangu zamani na anaamini ni mchezaji mkubwa mwenye ubora mkubwa ndani ya uwanja.
Nyota huyo wa Uganda alisema mijadala ya mashabiki kuhusu nani bora kati yao haimsumbui bali inampa motisha ya kuendelea kufanya vizuri zaidi akiwa Yanga.
Okello ambaye amejiunga Yanga Januari 2026 tayari amehusika kwenye mabao 16 ya Ligi Kuu Bara akifunga mabao tisa na kutoa asisti saba, huku Chama naye akiwa kwenye kiwango bora akiwa amehusika kwenye mabao 14 tangu arejee Simba.
Aidha, Okello amesema kitu kikubwa kwake si kushindana na Chama, bali kuhakikisha Yanga inashinda mechi zake na kutwaa ubingwa wa ligi msimu huu.


