

ANAANDIKA MENEJA HABARI NA MAWASILIANO WA KLABU YA SIMBA – AHMED ALLY
“….Hii ndio timu tunayotakiwa kujivunia, Timu ambayo imetutoa kwenye unyonge, imetutoa kwenye uteja na imeturejeshea heshima yetu na ukubwa wetu
Kutoka kwenye kufungwa mfululizo, Sasa hivi mpinzani anafurahia sare
Tumefanikiwa kuifanya Yanga kuwa kama Dodoma Jiji au Mtibwa ambazo hua zinashangalia sare dhidi ya Simba
Tumeshaondoa unyonge kilichobaki na kusimika ufalme na utawala wetu na hili haliko mbali Wana Simba
Kitu cha uhakika mpaka sasa ni kwamba Yanga hawana uwezo wa kutufunga kilichobaki ni Simba kuifunga Yanga..”


