
Hansi Flick: “Nitawaambia jambo… si jambo la kawaida, ni zito sana.”
“Asubuhi hii mama yangu alinipigia simu na kuniambia kuwa baba yangu amefariki dunia.”
“Nilikuwa najiuliza kama niwaambie wachezaji au la. Lakini wao ni kama familia yangu, hivyo niliwaambia.”
“Sitawasahau walichokifanya baada ya hapo. Kilikuwa kitu cha ajabu sana. Sitakisahau maisha yangu yote.”
“Nina furaha na fahari kubwa kwa kila mmoja. Kila mchezaji, kila mtu wa benchi la ufundi, kila mtu ndani ya klabu. Kwangu mimi, hii ni familia ya kweli.”



