
🇹🇿 Tanzania imewekeza zaidi ya dola milioni 12 (takribani Shilingi bilioni 1.56 za Kenya) ili kupata hadhi ya Mshirika Rasmi (Official Partner) na Mdhamini wa Utalii (Destination Sponsor) wa AFCON 2027, kupitia makubaliano makubwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Makubaliano hayo yanaipa Tanzania haki ya kutumia nembo na chapa rasmi za CAF na AFCON 2027, pamoja na kupata mwonekano mkubwa kimataifa kupitia matangazo ya CAF, majukwaa ya kidijitali na mitandao ya kijamii.
Ushirikiano huo unalenga kuitangaza Tanzania kama moja ya vivutio vikuu vya utalii duniani, huku ukitumia umaarufu wa soka la Afrika kuvutia watalii na wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali. 🇹🇿⚽🌍



