
Kipa wa Harambee Stars na Nairobi United, Farouk Shikalo, amekosoa ubora wa mpira rasmi unaotumika katika Ligi Kuu ya Kenya, akizitaka mamlaka za ligi hiyo kutafuta mbadala wenye viwango bora.
Shikalo amesema ubora wa mpira huo hauridhishi na hauendani na matarajio ya mashindano ya daraja la juu nchini Kenya.
“Ligi Kuu ya Kenya inastahili mipira yenye ubora kwa ajili ya soka zuri. Ubora wa mpira huu hauridhishi kabisa. Tafadhali jitahidini kutoa mipira yenye ubora zaidi,” amesema Shikalo.

