
Winga wa Chelsea, Mykhaylo Mudryk, amefichua kuwa ndoto yake ilikuwa kujiunga na Arsenal na kucheza katika Uwanja wa Emirates.
Mudryk amesema hakukuwa na juhudi za kweli za kumhamishia Arsenal, akidai kuwa wakala wake wa zamani alikuwa akilenga zaidi kupata fedha nyingi kupitia dili hilo.
Ameongeza kuwa hakujua kuhusu suala la kamisheni na maslahi ya kifedha yaliyokuwa nyuma ya mazungumzo hayo hadi baadaye alipokuja kuelewa kilichokuwa kinaendelea.

