

Saa 12:30 jioni, Yanga SC watakuwa uwanja wa KMC Complex wakiwakaribisha Namungo FC.
Yanga SC wanahitaji ushindi ili kurudi kuongoza msimamo wakati Namungo wanataka ushindi ili kujinasua kucheza PlayOff ya kushuka daraja.
Je, ni Wananchi ama Wauaji wa Kusini nani kuondoka na alama tatu?
Saa 3:00 usiku, matajiri wa jiji AzamFC watakuwa nyumbani Azam Complex wakiwakaribisha KMC FC wanaoburuza mkia.


