
Lionel Scaloni alistaafu kucheza soka mwaka 2015, kisha akaingia kwenye ukocha mwaka 2017 akitafuta nafasi na kupata leseni ya ukocha ya UEFA Pro.
Alisafiri kwenda Hispania kuhudhuria kozi hizo, akitumia uzoefu wake wa kucheza La Liga akiwa na Deportivo La Coruña na Mallorca.
Lakini unajua ni nani aliyekuwa akimfundisha Scaloni wakati huo?
Ni Luis de la Fuente Ndiye aliyekuwa akitoa mihadhara na mafunzo kwa Scaloni pamoja na makocha wengine, akimsaidia kukuza mbinu na falsafa yake ya ukocha.
Miaka 8 baadaye, De la Fuente ametumia uzoefu wake kuifikisha Hispania fainali ya Kombe la Dunia na cha kushangaza zaidi ni kwamba anayemsubiri upande wa pili wa fainali si mwingine bali ni Scaloni, mwanafunzi wake wa zamani.
Hawa makocha wote hawajawahi kufundisha vilabu vikubwa lakini mbinu zao kwenye timu za taifa zimewafikisha hapa walipo na kutambulika kama makocha bora kabisa duniani.
Tutashuhudia fainali ya Kombe la Dunia kati ya mwalimu na mwanafunzi wake. 🇪🇸❤️🇦🇷
