
#MICHEZO: Simba SC imeendelea kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu mpya baada ya kumtangaza rasmi kiungo mshambuliaji Bakari Misimu, mwenye umri wa miaka 18, kutoka Coastal Union.
Kijana huyo amesaini mkataba wa miaka miwili na Wekundu wa Msimbazi, huku akitajwa kuwa miongoni mwa vipaji vinavyopewa nafasi ya kukua na kuisaidia timu katika siku zijazo.
Misimu amejiunga na Simba akitokea Coastal Union, ambako alionyesha kiwango kizuri kilichovutia viongozi wa klabu hiyo.
Usajili wake unaonyesha dhamira ya Simba ya kuwekeza kwa wachezaji vijana wenye uwezo wa kuendelezwa na kuwa sehemu muhimu ya kikosi cha kwanza katika misimu ijayo.

