
Chama hicho cha wachezaji wa kulipwa duniani kimeeleza kusikitishwa na hatua ya viongozi wa mabingwa hao wa Ujerumani kumjadili hadharani Musiala na mkataba wake wakati huu akirejea uwanjani kutoka majeruhi.
FIFPRO imetaja hatua hiyo kama mbinu ya makusudi ya kumwekea shinikizo nyota huyo na wawakilishi wake kabla ya mazungumzo ya mkataba, ikisisitiza kuwa suala hilo linaathiri afya ya akili ya mchezaji na linapaswa kujadiliwa faraghani.
Chama hicho kimeikumbusha Bayern kuwa mikataba ipo ili iheshimiwe na majeraha hayatoi sababu ya kuijadili upya, huku kikiahidi kusimama bega kwa bega na Musiala pamoja na wachezaji wote wanaotimiza wajibu wao.

