Christos Tzolis: “Ni jambo la kushangaza sana kwamba mechi yangu ya kwanza ya Ligi Kuu England ilikuwa kwenye Uwanja wa Emirates!” 🤩
Nyota huyo mpya wa Arsenal amesema kumbukumbu ya kucheza mechi yake ya kwanza ya Premier League katika Uwanja wa Emirates bado ipo moyoni mwake na aliikumbuka tena alipokuwa akizungumza na familia yake.
“Nilikuwa nazungumza na familia yangu siku chache zilizopita kuhusu hilo. Ni moja ya kumbukumbu nzuri zaidi kuwahi kuwa nazo,” alisema Tzolis.
Winga huyo wa kimataifa wa Ugiriki pia hakusita kuusifu Uwanja wa Emirates, akieleza kuwa uliuvutia tangu mara ya kwanza alipocheza hapo.
“Niliupenda sana uwanja huo. Kila mara nilikuwa nikisema ni miongoni mwa viwanja bora zaidi ambavyo nimewahi kucheza,” aliongeza.
Sasa akiwa mchezaji wa Arsenal, Tzolis atakuwa na nafasi ya kuuita Emirates nyumbani kwake na kutimiza ndoto yake ya kucheza mbele ya mashabiki wa Gunners.
