
“Meja General Isamhuyo ndio Uwanja pekee wenye hadhi ya kuchezewa mchezo wa Kariakoo Derby baada ya Benjamini Mkapa
Bahati mbaya sana wote wanao ukataa Uwanja wa Meja Isamhuyo hawajafanya utafiti wa hali ya Viwanja Nchini Tanzania
Acha nikuambie kwanini Meja Isamhuyo ni chaguo sahihi
Azam Complex inaingiza mashabiki Elfu 4 tu, Tofauti ya Mashabiki Elfu 6 na Meja Isamhuyo, Hivyo tungepeleka mechi Azam Complex tungewaminya fursa mashabiki wengi, mfano Mechi ya Azam na Simba mashabiki wengi walibaki nje licha kununua Tiketi wakaambiwa Uwanja umejaa
Amaan Zanzibar inaingiza Mashabiki Elfu 14, tofauti ya yake na Isamhuyo ni Mashabiki wa Elfu 4 tuu hiyo ni tofauti ndogo sana
Unaweza kuitaja Kirumba Mwanza, au Sheikh Amri Abeid Arusha, Sokoine Mbeya vyote hivyo vinaingiza mashabiki chini ya Elfu 13 bado tuko pale pale kwenye idadi ndogo ya watazamaji
Kama Hitoshi kutokana na hali ya hewa hivi sasa, Viwanja hivyo havitabiriki sasa kwanini tuiweke Derby rehani??
Ukweli mwingine ambao hauzungumzwi ni kwamba Meja Isamhuyo ndio kiwanja cha pili Tanzania kuwa na Pitch nzuri ya Nyasi Asilia baada ya Benjamini Mkapa
Kwa hoja hiyo kwanini mechi namba moja ya Nchi isipigwe kwenye kiwanja cha pili kwa hadhi katika Taifa letu?
Karibuni sana Meja Isamuhyo naaamini mtafurahi mkifika!!”




