

Arsenal imekamilisha usajili wa winga wa kimataifa wa Ugiriki, Christos Tzolis, kutoka Club Brugge kwa ada ya euro milioni 40.
Tzolis ametia saini mkataba wa kuitumikia Arsenal hadi Juni 2031, na kuwa usajili wa kwanza wa klabu hiyo kuelekea msimu mpya.
Winga huyo anatarajiwa kuziba nafasi iliyoachwa na Leandro Trossard, ambaye ameondoka Arsenal na kujiunga na Beşiktaş.
Mashabiki wa Arsenal wana matumaini makubwa kuwa Tzolis ataleta kasi, ubunifu na mchango mkubwa katika safu ya ushambuliaji ya timu hiyo chini ya kocha Mikel Arteta.
⭐ Wewe unaupa alama ngapi usajili huu kati ya 1 hadi 10?

