baada ya klabu hiyo kutangaza rasmi kuwa beki wao tegemeo, William Saliba, atakuwa nje ya uwanjani kwa kipindi kirefu kutokana na majeraha, ingawa taarifa ya kutofanyiwa upasuaji inaleta ahueni ndogo.
Uchunguzi wa kina uliofanywa na madaktari umebainisha kuwa kwa sasa upasuaji hauhitajiki kwa ajili ya kutibu jeraha lake, bali mchezaji huyo ataanza mara moja matibabu chini ya uangalizi wa karibu.
Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na klabu hiyo, ilieleza wazi kwamba:
> “Matibabu ya William yataanza mara moja na kwa usimamizi endelevu wa jeraha lake, mchezaji huyu anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu.”
Kukosekana kwa staa huyo raia wa Ufaransa ni pigo kubwa kwa safu ya ulinzi ya Arsenal, huku kikosi hicho kikiwa kinahitaji huduma yake kwenye michuano migumu inayowakabili mbele.
Get well soon, Saliba

