Kamati ya tuzo ya Ballon d’Or imevunja ukimya kwa kutoa taarifa rasmi inayoweka wazi ukweli mchungu kuhusu uhusiano uliopo kati ya kubeba Kombe la Dunia na kushinda tuzo hiyo ya kifahari ya mchezaji bora duniani.
Kupitia tovuti yao rasmi, kamati hiyo imesisitiza kuwa mafanikio ya kimataifa pekee hayatoshi kumpa mtu ushindi wa tuzo hiyo.
> “Kushinda Kombe la Dunia hakukuhakikishii kushinda tuzo ya Ballon d’Or. Tangu 1995, wanne tu kati ya saba ndio wameweza kushinda Ballon d’Or baada ya ushindi wa Kombe la Dunia, ni asilimia 57 tu,”
– ilieleza taarifa hiyo.
Zaidi ya hayo, taarifa hiyo iliongeza kwa kusisitiza:
> “Ndiyo, kushinda Kombe la Dunia kunasaidia, lakini hakukuhakikishii Ballon d’Or. Ili kuishinda, unahitaji kuwa mchezaji bora wa msimu, sio wa Kombe la Dunia pekee.”
Nani unamwona akiibuka mshindi wa tuzo hii mwaka huu? 🍿
