

Hull City wamerejea rasmi kwenye Ligi Kuu England baada ya kusubiri kwa miaka tisa, kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Middlesbrough katika fainali ya play-off ya Championship iliyopigwa kwenye Wembley Stadium. 🏟️🔥
Bao la ushindi lilifungwa dakika za majeruhi na kuwapa “The Tigers” tiketi ya kurejea Premier League kwa kishindo baada ya msimu mgumu na wenye presha kubwa.
Kutokana na umuhimu mkubwa wa mchezo huo pamoja na drama nyingi zilizokuwa nje ya uwanja kabla ya mechi, haikushangaza kuona mwanzo wa mchezo ukiwa wa tahadhari kubwa huku timu zote zikicheza kwa uoga wa kufanya makosa.


