Tukio hili linatoka kwenye nyumba ya mapumziko iliyo karibu na pahala patakatifu pa Kombaru huko Karnataka India.
Chui alikuwa akimfukuza mbwa . Mbwa aliingia kwenye choo kupitia dirishani. Choo kilikuwa kimefungwa kwa nje.
Chui aliingia nyuma ya mbwa, na wote wawili wakakwama kwenye choo. Mbwa alipomwona chui, aliogopa na kukaa kimya kwenye kona moja. Hakuthubutu hata kubweka.
Ingawa chui alikuwa na njaa na alikuwa akimfukuza mbwa,lakini alishindwa kumla mbwa. Angeweza kumla kama chakula cha jioni kwa kumrarua mbwa kwa kumrukia mara moja.
Lakini wanyama hao wawili walikuwa pamoja katika pembe tofauti kwa karibu saa 12. Wakati wa saa hizi 12, chui pia alikuwa kimya.
Idara ya misitu na wanyapori ilimkaribia chui huyo na kumkamata kwa kutumia sindano maalum ya kumtuliza.
Sasa swali ni je kwanini chui mwenye njaa hakumdhuru mbwa wakati iliwezekana kirahisi???
Watafiti wa wanyamapori walijibu swali hili: Kulingana na wao, wanyama pori wanapenda sana kuwa uhuru. Mara tu wanapogundua uhuru wao haupo, wanaweza kuhisi huzuni kubwa, kiasi kwamba wanaweza kusahau njaa yao.
Motisha yao ya asili ya kula huanza kutoweka.
Uhuru na furaha vimeunganishwa. Uhuru wa kufikiri, kutenda na kuishi kwa namna wanayotaka.



