

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Dkt. Patrice Motsepe, amesema CAF haiwezi kuondoa Tanzania, Kenya na Uganda kuwa wenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.
Motsepe amesema amekuwa akisikia tetesi zikidai kuwa CAF inaweza kuzinyang’anya nchi hizo haki ya kuwa wenyeji wa mashindano hayo, akisema taarifa hizo zipuuzwe.
Amesema Tanzania, Kenya na Uganda zitaendelea kuwa wenyeji wa AFCON 2027, huku maandalizi ya mashindano hayo yakiendelea.
CAF pia imethibitisha kuwa nchi hizo tatu zimepangwa kuwa wenyeji wa mashindano hayo yatakayofanyika Juni 19 hadi Julai 17, 2027.
Dkt. Motsepe ameyasema hayo leo, Septemba 17, 2026, baada ya kuwasili nchini Tanzania kwa ajili ya kukagua maendeleo ya maandalizi ya mashindano hayo.
CAF ilitangaza kuwa katika ziara hiyo atatembelea Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam na kukutana na Serikali ya Tanzania kujadili maendeleo ya maandalizi.

