
Karim Adeyemi amesema kuwa kocha Hansi Flick ndiye sababu kubwa iliyomshawishi kujiunga na klabu hiyo.
“Hansi Flick ndiye sababu kuu iliyonileta hapa. Tumezungumza mara nyingi, na tangu mwanzo kabisa nilikuwa na imani kubwa kwake. Nimefurahi kuwa hapa na niko tayari kucheza nafasi yoyote katika safu ya ushambuliaji ili kuisaidia timu,” alisema Adeyemi.
Nyota huyo ameongeza kuwa lengo lake ni kushirikiana na wachezaji wenzake kuhakikisha timu inafanikisha malengo yote ya msimu.
“Niko tayari kufanya kila niwezalo kusaidia timu kufikia malengo yake. Bila shaka tunafahamu kuwa Ligi ya Mabingwa ni moja ya malengo makubwa, lakini ukweli ni kwamba kila mechi ni muhimu na tunapaswa kupambana ili kupata matokeo bora,” aliongeza.

