
🚨 BREAKING: Wydad AC yapinga taarifa za Sele Gomez kujiunga na Simba SC
Klabu ya Wydad AC imekanusha taarifa za mchezaji wake Sele Gomez kuhamia Simba SC kwa mkopo, ikieleza kuwa hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa kati ya pande hizo mbili.
_Wydad imesema Sele Gomez bado ni sehemu ya mipango ya klabu hiyo kuelekea msimu mpya na anaendelea kuwa na mkataba halali na timu hiyo._
> _Kwa sasa hakuna dili rasmi lililokamilika, huku ikisubiriwa kuona kama Simba itaendelea na mazungumzo zaidi au mpango huo utaishia hapo._

