_Klabu ya Manchester City imethibitisha kuwa kiungo mshambuliaji, Philip Walter Foden 26, raia wa England amesaini nyongeza ya mkataba mpya wa miaka minne wa kuendelea kusalia klabuni hapo mpaka Juni 2030._
_Akizungumza baada kusaini mkataba huo Foden amesema anajiona mwenye bahati kuwa sehemu ya kipindi cha kihistoria cha klabu hiyo kilichojaa mataji na kubainisha kwamba yeye na wachezaji wenzake wanaangazia zaidi siku zijazo kwa ajili ya kushinda mataji zaidi._
