Mshambuliaji Doumbia raia wa Mali mwenye miaka 19 kutoka AS korofina ya Mali amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba SC.
Msimu uliopita akiwa na AS Korofina ameibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Mali akifunga mabao 17 na Pasi za mwisho (Assist) 5.
Pia Doumbia amejumuishwa kwenye kikosi cha Mali chini ya miaka 20, na amefanikiwa kufunga mabao 20 kwenye mechi 26 alizocheza.

