Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi ametangaza ongezeko hilo leo Mei Mosi, 2026, katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Viwanja vya Maonesho ya Kilimo Kizimbani, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Amesema kiwango hicho kipya cha mshahara kitaanza kutumika Januari 2027 na kueleza kuwa hatua hiyo imezingatia hali ya uchumi wa nchi, gharama za maisha na kuwapatia motisha Wafanyakazi ili watekeleze majukumu yao kwa ufanisi.

