
Klabu ya Simba imeanza mchakato wa kunasa saini ya mshambuliaji wa Kimataifa wa Ivory Coast,Souleymane Fofana kuelekea dirisha kubwa la usajili.
Simba SC inaendelea kupigania saini ya staa na mfungaji bora pale ASEC Mimosas ambaye ni Fofana anayeongoza kwa ufungaji akifunga mabao 14 kwenye ligi ya Ivory Coast, lakini ikitokea ikashindwa basi kuna Kevin Bakare.
Bakare ndiye mshambuliaji mwenye namba nzuri kando ya Fofana na Simba SC imepata jina lake na sasa inapambana naye ikimweka tayari katika uwezekano wa kumsajili wakati wa dirisha kubwa la usajili.
Rekodi zinaonyesha, msimu huu Bakare ameshafunga mabao manane akiwa ndiye mfungaji bora namba mbili katika timu hiyo huku akitoa asisti tatu.





