
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Paul Makonda amesema uwanja wa Arusha ambao ni miongoni mwa viwanja vinavyotarajiwa kutumika katika Mashindano ya Soka Barani Afrika (AFCON) 2027 ni miongoni mwa viwanja bora vya mpira barani Afrika.

Mhe. Makonda amesema hayo wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba ambaye alifika kukagua maeneleo ya ujenzi wa uwanja huo jana Aprili 17, 2026.




