
Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limetoa rasmi viwango vya klabu bora kwa kipindi cha miaka mitano baada ya kumalizika kwa hatua ya makundi ya michuano ya CAF Champions League na CAF Confederation Cup msimu wa 2025/26.
Kwa mujibu wa CAF 5-Year Club Ranking, klabu kongwe ya Misri Al Ahly inaongoza kwa kujikusanyia jumla ya pointi 66, ikifuatiwa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini yenye pointi 58, huku EspΓ©rance Sportive de Tunis ya Tunisia ikishika nafasi ya tatu kwa pointi 53.
Katika nafasi ya nne ni RS Berkane ya Morocco ikiwa na pointi 52, ikifuatiwa na Pyramids FC ya Misri yenye pointi 48, wakati Al Hilal ya Sudan

na Zamalek SC ya Misri wakishika nafasi ya sita na saba mtawalia kwa pointi 39 kila mmoja.
Simba SC na Yanga Zaipeperusha Bendera ya Tanzania
Klabu za Tanzania zimefanikiwa kuingia ndani ya klabu 10 bora barani Afrika, huku Simba SC ikishika nafasi ya nane kwa pointi 38, na Young Africans SC (Yanga) ikichukua nafasi ya kumi kwa pointi 35.

Hii ni hatua kubwa kwa soka la Tanzania, ikionyesha namna klabu zake zimekuwa zikifanya vizuri katika mashindano ya CAF kwa miaka ya karibuni, licha ya changamoto za ushindani mkubwa kutoka kwa vigogo wa soka barani Afrika.
CAF 5-Year Club Ranking 2025/26
- 1. Al Ahly β pointi 66
- 2. Mamelodi Sundowns β pointi 58
- 3. EspΓ©rance Sportive de Tunis β pointi 53
- 4. RS Berkane β pointi 52
- 5. Pyramids FC β pointi 48
- 6. Al Hilal β pointi 39
- 7. Zamalek SC β pointi 39
- 8. Simba SC β pointi 38
- 9. USM Alger β pointi 37
- 10. Young Africans β pointi 35
Maana ya Nafasi Hizi kwa Soka la Tanzania
Kuwepo kwa Simba na Yanga ndani ya klabu 10 bora Afrika kunadhihirisha ukuaji wa soka la Tanzania katika ramani ya kimataifa. Hii inaongeza heshima ya ligi kuu ya Tanzania, kuvutia wadhamini, wawekezaji pamoja na kuongeza mvuto wa wachezaji wa kimataifa kujiunga na klabu za ndani.
Pia viwango hivi vinaweza kusaidia timu za Tanzania kupata nafasi nzuri zaidi kwenye droo za mashindano ya CAF, hali inayoweza kuongeza uwezekano wa kufika mbali zaidi katika misimu ijayo.
Chama Lako Lipo Namba Ngapi?
Kwa mashabiki wa soka, je klabu yako iko nafasi ya ngapi katika viwango hivi vya CAF? Je unaamini Simba na Yanga wanaweza kupanda zaidi na kuingia ndani ya klabu tano bora Afrika msimu ujao?
Endelea kufuatilia tovuti yetu kwa habari za michezo, uchambuzi wa kina, matokeo ya mechi, ratiba, msimamo wa ligi na taarifa zote muhimu za soka la Tanzania na Afrika kwa ujumla.




