Tayari tamko la mwaka limetoka; Nilipokuwa Nasoma Masoko Na Mauzo (Sales and Marketing) Nilifundishwa Kitu Kimoja Na Mwalimu Wangu.
Aliniambia Kwamba “, When A Customer Reject Your Product, Knows That He/She Has Not Reject Your Product As It Is, But Your Offer”
Alimaanisha Kwamba, Pale Mteja Atakapoikataa Bidhaa Yako, Hajaikataa Bidhaa Kama Bidhaa Ila Amekataa Ofa Yako, Yaaani Namna Ulivyotaka Kumuuzia Hiyo Bidhaa.
Baada Ya Miaka Mingi Kupita, Nimejifunza Kitu Kimoja Kikubwa Sana, Nimejifunza Kwamba Kanuni Za Masoko Na Mauzo Ni Sawa Na Kanuni Za Utongozaji.
Ndio Maana Dan Bilzerian Ambae Ni Mmoja Kati Ya Watongozaji Mahiri Aliwahi Kusema Hivi
“Laws Of Seduction And That Of Making Money Through Business Are The Same “ Yaani
Kanuni Za Utengenezaji Wa Fedha Kupitia Biashara Hazitofautiani Na Kanuni Za Utongozaji.
Hii Ni Kwa Sababu Kwenye Biashara UNAUZA BIDHAA YAKO… Na Kuifanya Ikubaliwe Lakini Kwenye Kutongoza UNAJIUZA WEWE Ili Kumfanya Unaemtongoza Akukubalie.
Zoezi ni Lilelile Linahusu Uuzaji Na Kanuni Zake Ni Zilezile.
Unapomuuzia Mteja Kitu Anaweza Kukataa, Sio Kwa Sababu Hakitaki, Ila Kwa Sababu Hajashawishika
Kwahiyo, Majibu Yake Yooote Ya “Sina Hela, Bei Yako Kubwa, Nitakuja Wakati Mwingine, Ngoja Nikafikirie”
Hayo Yoote Yana Maanisha Kuwa “Hujanishawishi Vya Kutosha Kiasi Cha Mimi Kukupa Hela Yangu”
Ndio Maana Mteja Anaweza Akaacha Kununua Bidhaa Kwako Akaenda Kununua Kwa Mwingine.
Hiyo Yoote Huthibitisha Kwamba Wewe Hujamshawishi
NB; Tuwe Wabunifu Kwenye Ufanyaji Wa Biashara Ili Kutengeneza Wateja Zaidi



