Sema 2Pac alikuwa mwamba sana.
Kwanza muvi inaanza alikuwa kwenye mahusiano na bonge moja la manzi la kuitwa Jada Pinket ila by then kila walipokuwa wakiulizwa walisema walikuwa marafiki tu.
Will Smith alimmaindi sana mchizi lakini hakuwa na jinsi kwani hata naye Jada alisema jamaa alikuwa rafiki tu, tena wa kawaida, yaani marafiki wa kawaida wakawa wanakumbatiana na mahaba tele.
Siku zikasonga.
Baadaye Pac akaweka bayana kwamba alikuwa kwenye mahusiano na mwanamama Janeth Jackson. Huyu ni mdogo wake na Michael Jackson.
Mahusiano hayo yalimkasirisha sana MJ lakini hakuwa na jinsi, mdogo kashapenda ilikuwa ni lazima atulie pembeni watu waendeleze mahaba yao. Mahusiano hayo yakawafanya kuigiza muvi iitwayo Poetic Justice.
Sasa baada ya siku kwenda mbele huku jina lake likiwa kubwa, MJ akakunjua, akasema anatoa baraka zote kwa Pac kuendelea kujilia mdogo wake na kwa sababu miaka hiyo jamaa alikuwa naye maarufu kama MJ, akataka afanye naye ngoma moja. Yaani shemeji na kaka wa mchumba ndani ya traki moja.
Miadi ikapangwa. Pac akamwambia mpaka mama yake kwamba alikuwa amepata nafasi ya kufanya ngoma na MJ. Haikuwa rahisi kuamini kwani MJ hakuwa mtu wa kawaida hata kidogo, lilikuwa ni bonge moja la dude.
Siku ya kurekodi ikafika.
Chap Pac akaruka mpaka studio akiwa na wapambe wake, yaani kichwani mwake kulikuwa na mambo kibao. Alipofika studio, MJ hakuwemo.
Kila kona alipoangalia.
Mwamba hakuwemo.
Hilo likampa maswali, inakuwaje hayumo humo na wakati muda wa kurekodi ulifika?
Alipoulizwa.
Akajibiwa wewe ingiza verse yako, yeye akija ataingiza yake.
Pac akashangaa!
Yaani nina shauku ya kuonana na msela halafu leo unaniambia niingize verse bila yeye kuwemo!
Haiwezekani.
Pac akakataa na kusema na wapambe wake.
Akamchukia sana MJ kwa kile kitendo.
Pac alijiona naye yupo juu kama MJ na hakutakiwa kuingiza verse bila kuonana naye.
Basi ngoma ya pamoja ikashindikana japokuwa watu waliisubiria sana.
Mwisho wa siku, kundi la The South Side Crips likatumwa na Diddy kwenda kummaliza mwamba.
Mwisho wake ukawa huo, kupigwa risasi nyingi tu ndani ya gari



