Wakati Ronaldo yupo Saudi Arabia anasakata kabumbu, upande wa pili anajiandaa kurudi kwao Ureno jijini Lisbon kuanza maisha mapya nchini kwake. Sasa stori ambazo zimesambaa ni kwamba shule moja iitwayo St. Julian imekataa watoto watano wa mwanasoka huyo kusoma shuleni hapo.
Hiyo ndiyo shule private namba moja Ureno kwa kusomwa na wanafunzi wa kitajiri na hata wale ambao wazazi wao wana nguvu, kwa nini wamewakataa?
Ni kwa sababu ya ulinzi wa watoto wengine. Kwa kitendo cha watoto wa Ronaldo kusoma hapo inamaanisha waandishi watawafuatilia sana kitu ambacho kitahatarisha hata usalama wa wanafunzi wengine ambao wazazi wao wana nguvu na utajiri mkubwa



