Steve Jobs alikufa akiwa na umri wa miaka 56 kwa maradhi ya kansa ya kongosho akiwa bilionea mwenye utajiri wa dola bilioni 7. Baadhi ya maneno yake ya mwisho kabla ya kufa kwake ni;
1. Nikiwa mgonjwa kitandani kumbukumbu ya maisha yote niliyoishi imenijia na kutambua kwamba utajiri na umaarufu hauna maana yoyote mbele ya kifo.
2. Walau tunapoingia utu uzima tunaanza kuelewa kwamba saa inayouzwa 3,000 na ile inayouzwa 300,000 zote huonyesha masaa sawa. Haijalishi utaendesha gari ya milioni 5 au ya milioni 500 kikubwa unafika unakotaka inatosha.
3. Usijikite tu kusomesha wanao ili baadaye wawe matajiri, wafundishe pia kuthamini na kufurahia vitu walivyonavyo ili baadaye watakapokua wasihangaike kutafuta furaha kwenye vitu ambavyo hawana.
4. Kula chakula kama dawa vinginevyo utaishi kwa kula dawa kama chakula.
5. Akupendaye hatokuacha kamwe hata kama utakuwa na sababu 100 za kuachwa. Siku zote atakuwa na sababu ya kuwa na wewe.
6. Kuwa mtu na kuwa na utu ni vitu viwili tofauti.
7. Ukitaka kusafiri kwa kasi safiri peke yako lakini ukitaka kufika mbali tafuta wa kwenda naye.



