Nitakuambia ukweli na siri wala sitakuchaji hata sumni wala shilingi yoyote. Vitu tulivyopewa bure tunavitoa Bure. Wala usinipe sifa yoyote Kwa maana sistahili sifa. Wala usinishukuru Bali mshukuru Mungu wako aliyekuumba.
Niite The legend, Mwalimu asiye wa Mshahara lakini asiyepungukiwa na chochote.
Kila mtu hupenda kufanikiwa Kwa kila Jambo alifanyalo. Binadamu wengi Kama sio wote hupenda mambo mazuri. Kwayo huyaita mafanikio. Hata hivyo kila mtu anamafanikio yake kulingana na Yale ayapendayo,
Lakini mafanikio ili kuyafikia kunahitaji mchakato Fulani. Leo Taikon atajadili Jambo moja nyeti katika Mafanikio ambalo ni kanuni ya “ONDOKA” au “ACHA” na ili uondoke au uache itakupasa usiwe na UOGA. Ukiwa muoga huwezi kuondoka au kuacha baadhi ya vitu au mambo. Utaishi Kwa mazoea na kuogopa vitu ambavyo havipo.
Huwezi kufanikiwa katika Jambo lolote Kama hujaitumia kanuni hiyo. Kanuni hiyo ni moja ya nguzo muhimu ya mafanikio.



