1. Mtu muhimu sana
2. Mtu wa muhimu
3. Mtu ambaye hana umuhimu wowote
4. Mtu wa kawaida.
WEWE JE UCHUKULIANE NA WATU KIVIPI?
Jitahidi sana kuwathamini watu wote. Yesu alikuwa anawapenda kimakundi lakini aliwathamini wanafunzi wote. Yesu alikuwa karibu sana na wale watatu yaani Petro, Yakobo na Yohana. Pia akawa na wale wote kumi na mbili. Kuna kipindi tunaona aliwatuma sabini LAKINI aliweza kuwahudumia kila mmoja na madhaifu yake. Hata Yuda aliyemsaliti pamoja na wizi aliokuwa nao alimhudumia vizuri tu kama binadamu.
Hivyo nakushauri ishi vizuri na watu sababu kesho utamhitaji lakini pia Mungu atakubariki.
UTAJUAJE NAFASI YAKO KWA MTU?
1. MTU WA MUHIMU SANA
Ikiwa wewe ni mtu wa muhimu sana kwa mtu, mara kwa mara ataonyesha kukutafuta hata kwa simu, na hata kama hana cha maana cha kuongea atakusalimia tu.
Ukimpigia simu mtu anayekuona wewe ni wa MUHIMU SANA yuko tayari kupokea muda wowote. Na iwapo akiwa busy atakuwa tayari hata kukatisha kikao kidogo ili akujibu kuwa yupo kikao na atakutafuta baadae.
Kama wewe unaonekana kwa mtu kuwa ni wa muhimu sana basi ujue kuwa huyo mtu ameamua kuwa nawe kwa upendo bila hata kuhesabu madhaifu yako. Atakueleza ukweli ukikosea au ukimkosea ili kukusaidia na kuendeleza upendo halisi alionao kwako.
Iwapo wewe ni wa MUHIMU sana kwa mtu basi ujue huyo mtu yupo tayari kushirikiana na wewe kwa jambo lolote na anajisikia furaha kujitoa kwako. Hata ukimpigia simu USIKU SANA atajitahidi apokee ili kujua kuna jambo gani limekusibu.
JINSI YA KUENDELEZA UMUHIMU WAKO SANA KWA HUYO MTU.
A. Uwe muwazi kwake na mkweli kwake.
B. Onyesha upendo na kujali.
C. Anapokuelekeza usiumie bali ujue anakupenda kabisa, hivyo kubali maelekezo.
D. Onyesha ushirikiano naye.
ANGALIZO
Jitahidi usimpoteze sababu anajitoa kwako kwa UPENDO. Huyo ndiye ndugu wa ukweli wa moyo.
2. MTU WA MUHIMU.
Ikiwa wewe ni wa muhimu kwa mtu, huyo mtu atakuwa karibu nawe hasa katika umuhimu wa jambo husika.
Mtu atakutafuta na kuonyesha thamani yako kwa sababu huwa unamsaidia katika jambo hilo. Mara nyingi mahusiano yako wazi tu kuwa anakuhitaji kwa jambo husika.
Ukimtafuta hata kwa simu atapokea tu kwa haraka lakini hata hasipo pokea kwa sababu ya mazingira yake huwa hana mzigo mkubwa wa kukutafuta lakini atakutafuta ili kulinda kile anakipata kwako au anatarajia kukipata kwako.
Kwake, wewe ni wa muhimu lakini sio wa maana sana ndio maana kikikosekana cha muhimu kwake kutoka kwako na umuhimu wako kwake unakwisha. Kama kazini kwako kuna mnufaisha yeye na ukapoteza kazi basi ndio itakuwa mwisho wa umuhimu wako.
Usikubali kumpoteza kwa wepesi sababu maisha ni mtandao yeye anakuhitaji pia nawe utamhitaji katika mambo yako.
JINSI YA KUENDELEZA UMUHIMU WAKO KWA MTU
A. Jitahidi usipoteze kile huwa ananufaika au anachotarajia kutoka kwako.
B. Anapopata hitaji la jambo analotaka kwako jitahidi umshughulikie mapema.
ANGALIZO
Usifanye kitu zaidi ya uwezo wako ili tu uendelee kutunza umuhimu kwake. Ukifanya hivyo utakuwa MNAFIKI bali unaposhindwa katika mambo yake mwambie ukweli.
3. MTU AMBAYE HANA UMUHIMU WOWOTE.
Ikiwa wewe hauna umuhimu wowote kwa mtu itajulikana tu. Kwanza atataka ujue kuwa wewe hauna umuhimu kwake kwa vitendo. Iwapo ukimtafuta, hawezi kupokea au hata kujibu meseji. Hata akikujibu zitakuwa zimepita siku kadhaa.
Ukiwa hauna umuhimu wowote, wewe ndiye utakuwa unamtafuta tu na wala sio yeye. Ukimtafuta, yeye hudhani kuwa unamsumbua sababu hauna maana yeyote.
Kimsingi ni kuwa kama hauna umuhimu wowote basi ujue kuwa hauna thamani yoyote kwake. Mtu anayekuona wewe hauna umuhimu kwake akikutafuta ni kwa sababu tu amekukumbuka lakini sio kwa sababu una maana kwake.
Kama mwanzoni alikuwa anakuona wa muhimu na mabadiliko yametokea unaona hana ushirikiano nawe UJUE kwa sasa wewe HAUNA UMUHIMU KABISA.
ILI UWE SALAMA NA KWA MTU ANAYEKUONA HAUNA UMUHIMU KABISA KWAKE UFANYEJE.
A. Usiwe karibu sana na yeye. Utaumia moyo wako.
B. Usiwe na maamuzi ya haraka kumtupa mbali na usimwondoe na usi mblock kwa haraka kwenye mawasiliano sababu bado shida ni yake sio yako. Ingekuwa shida ni yako angekueleza ukweli.
C. Kama una upendo na ukiona amani ya moyo na ukaona haonyeshi kuona umuhimu wako mwambie hata kwa meseji na baada ya hapo endelea na maisha yako usimrudie ili siku hakikuhitaji aanzie pale ambako hakuona umuhimu wako.
D. Usiumie moyo, jilinde sana unapohusiana na mtu ambaye haoni umuhimu wako.
ANGALIZO
A. Kuwa makini usifanye maamuzi ya kuharibiana sababu kuna siku anaweza akajirudi na akawa rafiki wa karibu sana kuliko mwanzo.
B. Na pia kuwa makini, usilazimishe kuendelea kuwa naye au kuwasiliana naye sababu anaweza kukufedhehesha na kukuaibisha kabisa.
4. MTU WA KAWAIDA SANA.
Kama wewe unaonekana kuwa mtu wa kawaida sana kwa mtu basi ujue ni jambo jema. Ukiwa mtu wa kawaida kwa mtu ni nzuri sababu mtu anakuwa hana shida nawe wala hana hila nawe.
Ukiwa mtu wa kawaida hata ukimtafuta huyo anayekuona wa kawaida anaitikia tu sababu hana chochote anachohitaji kwako.
Mtu anayekuona wa kawaida mfanye tu aendelee kukuona wa kawaida hata kama wewe unajiona sio wa kawaida.
NB.
Katika namna zote hizo jinsi unavyoonekana kwa mtu jitahidi sana kuruhusu MOYO WAKO KUWA SALAMA na kuchukua MAAMUZI SAHIHI unapokabiliana na mazingira hayo.
Peleka nguvu katika kujipigania maisha yako na usiwe na chuki na mtu.
Binadamu anaweza kubadilika muda wowote hivyo uwe makini katika dunia hii.
Mtu anapokuchulia vibaya leo basi usipambane naye bali pambania maisha yako tu.
Usipoteze mahusiano na wengine kwa sababu kuna mtu alikuchukulia wewe kuwa HAUNA UMUHIMU KABISA.



