KATIKA mahojiano, nguli wa Mpira wa miguu Samuel Etoβo amesema kuwa Anachofanya Messi kwenye mechi hazifiki hata nusu ya kile alichofanya mazoezini.
Wakati wa mazoezi yake ya kwanza na kikosi cha kwanza cha Barca, kocha Rijkaard alimuunganisha Eto’o, Messi na Ronaldinho na katika dakika 15, Messi alifunga mabao 5.
Ronnie (Ronaldinho) na Eto’o walitazamana na wakakosa la kusema. Ustadi mwingi ambao Ronaldinho alikuwa akifanya kwenye michezo, Messi aliweza kufanya hivyo akiwa na umri mdogo sana lakini hakufanya hivyo kwenye michezo kwa sababu ya heshima na kwa sababu jambo la msingi pale Barca lilikuwa ni mafanikio ya timu sio mtu binafsi. Messi ndiye mchezaji bora zaidi.alimalizia Eto’o



