
Kumekuwa na lawama nyingi zikielekezwa kwa Arsenal kuhusu kushindwa kumalizana na straika matata Victor Gyokeres, lakini ukweli wa mambo ni tofauti kabisa – shida iko kwa Rais wa Sporting CP, Frederico Varandas.
✍️ Tatizo Halisi: Rais Hataki Dili na ArsenalKwa mujibu wa taarifa, Rais Varandas hana uhusiano mzuri na Arsenal, lakini ana mahusiano mazuri na Manchester United. Awali, wakati Man United walionesha nia ya kumsajili Gyokeres, kifungu cha kuachia kilikuwa €60 milioni tu, lakini baada ya Gyokeres kukataa kujiunga na Man United, bei ilipandishwa ghafla.
Bei Yabadilika kwa Arsenal Tu
Baada ya Arsenal kuonesha nia, bei ilipandishwa hadi €80 milioni. Arsenal walijibu kwa kutoa €65 milioni + €15 milioni kama nyongeza, jumla €80 milioni, lakini pia ikakataliwa.Sasa Rais anataka zaidi ya €100 milioni + nyongeza, huku Arsenal wakitoa ofa ya mwisho ya €80M + €20M = €100M, lakini bado Varandas amekataa!
Gyokeres Mwenyewe Hataki Man United
Victor Gyokeres amechoshwa na hali hiyo na amekataa kabisa kujiunga na Man United. Kwa sasa anasisitiza kuwa hataki kurudi Sporting CP, na yuko tayari kujiunga na klabu yoyote Ulaya isipokuwa Man United, hata kwa mkopo.Gyokeres ameweka wazi kuwa amechoka na hali hiyo, na tayari ametishia kutorejea Sporting.
️ Hata wewe ungekuwa Arsenal ungefanyaje?
Kwa sasa, Arsenal imekata tamaa kabisa, licha ya kuwa tayari kulipa pesa kubwa, lakini ukuta mkubwa ni Rais wa Sporting CP mwenyewe ambaye ameweka mbele mahusiano ya Man United kuliko maslahi ya mchezaji na klabu nyingine.



