Vijana wengi wana ndoto kubwa za mafanikio, lakini ndoto pekee hazitoshi. Ili kufanikisha jambo lolote maishani, unahitaji kuwa na:
1. Malengo Yenye Mwelekeo Jiulize, unataka kuwa nani baada ya miaka 5 au 10? Weka malengo yanayoweza kupimika na kuyafanyia kazi kila siku.
2. Nidhamu na Uvumilivu – Si kila kitu kitafanikiwa mara moja. Nidhamu ya kufanya kazi kwa bidii hata pale unapojisikia kuchoka ndiyo inayoleta matokeo makubwa.
3. Elimu na Maarifa – Kusoma vitabu, kutafuta maarifa mapya, na kujifunza kutoka kwa waliofanikiwa hukupa mtazamo mpana wa maisha.
4. Marafiki Wanaokutia Moyo – Mtu anayekuzunguka ana athari kubwa kwenye maisha yako. Chagua marafiki wanaokuinua, si wanaokuvuta chini.
5. Afya na Maadili – Huwezi kufanikisha lolote ikiwa huna afya njema. Kula vizuri, fanya mazoezi, na epuka tabia mbaya zinazoweza kukuharibia maisha.
Vijana tunaweza kufanikisha ndoto zetu kwa njia bora zaidi tukizingatia haya



