Ni tarehe 10 Mwezi wa 12 mwaka 2022 . Ni kwenye Dimba la Al Thumama pale Doha ,Qatar.
Umemalizika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Dunia kati ya Timu ya Taifa ya Ureno dhidi ya Morocco. Youssef En -Nesyri alishaijeruhi Ureno.
Yees ni Morocco ipo mbele ya bao 1 dhidi Ureno . Bao la Kichwa safi kabisa kutoka kwa Youssef na Mwanaume Facundo Tello wa Argentina anapuliza kipyenga na kumaliza mchezo huku ureno ikipoteza mbele ya mashabiki wapatao 44,198.
Ni furaha kwa kocha Walid Regragui wa Morocco lakini ni lawama kubwa kwa kocha wa Ureno Fernando Santons. Kwanini amuweke Ronaldo kwenye dakika ya “82 ” Why? .
Baada ya Mchezo ule mashabiki wa timu ya Taifa ya Morocco walifanyiwa mahojiano nje ya uwanja na haya ndio yalikuwa majibu yao
Binti mdogo ambaye alikuwa ni shabiki wa Morocco alipoulizwa kuhusu mchezo alijibu ️”Yuko wapi Ronaldo, Analia kwenye gari lake , Masikini Ronaldo ”
Raia mwingine wa Morocco alivyoulizwa kuhusu mchezo na yeye alijibu ️”Yuko wapi Ronaldo, yuko wapi Cristiano Ronaldo ”
Mwingine akajibu “Morocco hii njia ( nusu fainali ) , Ureno uwanja wa ndege “
Kejeli zilikuwa nyingi mnoo kwa Cristiano Ronaldo kutoka kwa mashabiki wa timu ya Taifa ya Morocco.
Tarehe 10 Mwezi wa 9 Mwaka 2023 ikiwa ni siku kadhaa baada ya kutokea tetemeko kubwa kwenye Nchi ya Morocco ambalo lilisababisha vifo vya watu zaidi ya 2000 na wengine kujeruhiwa .
Cristiano Ronaldo alitoa moja ya Hotel yake pale Morocco kwenye jiji la Marrakech inayoitwa PESTANA CR7 .
Hotel hiyo yenye vyumba 174 vya starehe na ufahari Cristiano Ronaldo alitoa bure kwa familia ambazo zilikosa makazi.
Na Cristiano Ronaldo alitoa ujumbe huu ️” Natoa pole kwa familia na marafiki kwa wale wote ambao wamepoteza maisha yao kwenye Tetemeko ndani ya Morocco . Natuma maombi yangu kwa raia wote wa Morocco kwenye kipindi hichi kigumu ”



