
Dakika 90: Yanga vs Kagera Sugar
Ulikuwa mchezo wa wazi kila timu ikichagua namna ya kupigana vita yake:
Yanga waliamini kwenye possession (umiliki wa mpira) huku Kagera wakiwekeza nguvu kwenye kuzuia wakisubiri kushambulia kwa counter attacks
Yanga kwenye Rest Defence imekuwa ndio utaratibu wa Ramovic kwa sasa (Job Aucho Bacca), movements za Mudathir Aucho na Aziz Ki katika mwa kiwanja ziliwapa tabu Kagera iliyokuwa kwneye midblock ya 5-4-1
Mzize akitoka pembeni na kuingia ndani kuungana na Dube na kuwa namba 9 wawili akimuachia Boka nafasi ya kuoverlap,
Yanga kwenye build-up ya 2-2-4-2 ambayo haikuwa na manufaa kwani Kagera hawakufanya pressing wakiamini ni kazi bure wakabaki kwenye muundo wao wa uzuiaji na hawakufunguka
Ramovic aliivunja vipi lowblock ya Melis Medo:
i. Ball Progression – tukimiliki mpira tunapiga pasi kwenda kwenye half ya mpinzani, na kukwepa kwa namna yoyte ile kupiga backpass..



