
Klabu ya Singida Black Stars imefikia makubaliano na klabu ya Wydad AC ya nchini Morocco ya kumuuza mchezaji Selemani Mwalimu kwa mkataba wa moja kwa moja kwa dau tulilokubaliana (undisclosed fee).
Sehemu ya makubaliano hayo ni klabu ya Singida BS kupata asilimia 10% ya mauzo ya baadae (sell-on) endapo Wydad AC itamuuza kwenda klabu nyingine.



