Takriban watu ishirini wameripotiwa kufariki dunia huku mmoja akinusurika kifo baada ya kuhusika katika ajali ya ndege kaskazini mwa Sudan Kusini.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Waziri wa Habari na Mawasiliano wa Jimbo la Unity Gatwech Bipal, ndege hiyo ilikuwa ikisafirisha abiria kutoka Jimbo la Unity hadi Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini, ikiwa na watu
21.
“Leo saa 10:30 a.m. (0830 GMT), ndege ilianguka kwenye uwanja wa ndege wa Unity Oil. Watu 21 walikuwa ndani, wakiwemo wafanyakazi,” alisema Bipal kwa njia ya simu na Xinhua Jumatano.
Inaripotiwa kuwa aliyenusurika kifo yuko katika hali mahututi na kwa sasa yuko chini ya uangalizi mkali wa matibabu.
Kisa cha ajali hiyo bado haijawekwa wazi.



