
Golikipa wa Simba Aishi Manula ameshindwa kusafiri na timu kwenda nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wao wa pili hatua ya makundi michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Cs Constantine ya Algeria.
Taarifa kutoka Simba imeeleza kuwa mchezaji huyo amepata changamoto ya kiafya akiwa uwanja wa ndege tayari kwa safari.
“Mlinda mlango Aishi Manula ameshindwa kuendelea na safari baada ya kupata changamoto ya kiafya dakika chache kabla ya kuanza safari ya kuelekea nchini Algeria tukiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Simba watashuka dimbani Desemba 08 nchini Algeria ukiwa ni mchezo wa pili baada ya kushinda mchezo wa kwanza dhidi ya Bravos.


