
Kiungo wa Fiorentina, Edoardo Bove ambaye jana Jumapili, Desemba 1, 2024 alizimia uwanjani wakati wa mchezo kati ya klabu hiyo dhidi ya Inter Milan amerejewa na fahamu na anaendelea vizuri huku akiwa chini ya uangalizi wa madaktrari ikiwa zaidi ya masaa 13 tangu apoteze fahamu.
Hizi ni habari njema kwa wapenzi wa soka baada ya tukio la jana kuzua simanzi miongoni wachezaji wa timu zote mbili wakati wa mchezo wa Serie A ambapo mpaka wakati huo hakuna timu iliyoona lango la mwenzake kabla ya mwamuzi kuahirisha mchezo.



