
7 ndio idadi ya mechi ambazo Manchester City wamecheza bila kupata ushindi wakipoteza 6 na kutoa sare mchezo mmoja,
Liverpool leo wameendeleza machungu kwa City baada ya kuwabamiza goli 2-0 magoli ya Gakpo ’12 na Salah ’78 kwa mkwaju wa penati yalitosha kuipa Liverpool alama 3.
Wakati majirani zao wakiteseka Manchester United wao mwendo mdundo wakipata ushindi wa goli 4-0 dhidi ya Everton, ukiwa ni ushindi wa kwanza kwenye ligi chini ya Mwalimu mpya Ruben Amorim magoli ya Rashford ’34 ’46 na Zirzkee ’41 ’64.
Matokeo ya michezo mingine;
Chelsea 3-0 Aston Villa
Tottenham 1-1 Fulham
Pep vipigo vimezidi kisukari kimepanda?



