Halikadhalika, Mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 17 Mkazi wa Kijiji cha Kilambo, mwanafunzi wa kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Ikimba amehukumiwa kifungo cha nje miezi 12 pamoja na kumlipa fidia mhanga kiasi cha shilingi laki mbili [200,000/=] kwa makosa mawili kubaka na kumpa mimba mwanafunzi alilolifanya kwa binti mwenye umri wa miaka 17 mwanafunzi kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Ikimba.
Hukumu hiyo imetolewa katika Mahakama ya Wilaya ya Kyela na Mhe.Hakimu Paul Barnabas – SRM Oktoba 24 2024 na Mwendesha mashitaka wa Jeshi la Polisi Mkaguzi Msaidizi Bihemo Mayangela Dawa. Hukumu hiyo ni kwa mujibu wa kifungu cha 130 kifungu kidogo cha kwanza na cha pili (e) na kifungu cha 131 kifungu kidogo Cha pili (a) vyote vya sheria ya kanuni ya Adhabu pamoja na kifungu cha 60A kifungu kidogo cha tatu cha sheria ya elimu mshitakiwa alitenda kosa hilo Julai 15, 2024 baada ya kumlaghai mwanafunzi mwenzie kuwa atamuoa baada tu ya kumaliza masomo yake.
Hukumu/Adhabu hizo zimetolewa kwa mujibu wa sheria ili iwe fundisho kwa watu, wanafunzi wengine na vijana wengine wenye tabia na wanaofikiria kufanya vitendo kama hivyo kwa watu wengine, wanafunzi na mabinti wadogo.
Jeshi la Polisi linaendelea kutoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana hasa katika utoaji ushahidi mahakamani ili kesi ziweze kupata mafanikio. Pia linatoa shukrani kwa vyombo vyote vya haki jinai kwa ushirikiano mkubwa unaotolewa ili kuhakikisha haki inatendeka dhidi ya washitakiwa/watuhumiwa wa makosa mbalimbali ya jinai.
Mbeya: Kesi 1072 zimefikishwa Mahakamani ndani ya Oktoba 2024
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea na jitihada mbalimbali za kubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu hali inayopelekea kukamata watuhumiwa wa makosa mbalimbali na kuwafikisha mahakamani kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.
Kwa kipindi cha mwezi Oktoba, 2024 jumla ya kesi 1072 zilifikishwa mahakamani ambapo kesi 195 zilipata mafanikio kwa watuhumiwa kukutwa na hatia na kuhukumiwa vifungo jela huku kesi 751 bado zipo mahakamani zikiendelea katika hatua mbalimbali.
Miongoni mwa kesi zilizopata mafanikio mahakamani kwa kipindi cha mwezi Oktoba, 2024 ni pamoja na ile ya shambulio la aibu, kubaka na kumpa mimba mwanafunzi na unyangβanyi wa kutumia silaha.



